Mambo 5 Ya Kuepuka Mara Tu Unapochumbiwa
Kuna Mambo Kadhaa Ambayo Msichana Anatakiwa Kuwa Makini Nayo Katika
Kuhakikisha Uchumba Wake Unadumu Na Kufikia Hatua Ya Kuolewa Na Kwenda
Kuanza Maisha Mapya.
Yapo Mengi Lakini Nitagusia Matano Ambayo Kwa Utafiti Wangu Ndiyo
Yamekuwa Yakiwafanya Wengi Wakimbiwe Na Wachumba Wao Na Kuachwa Wakilia.
1. Mazoea Na Wanaume
Wapo Ambao Wamejikuta Wakiachwa Solemba Kufuatia Tabia Zao Za Kuwa Na Mazoea Ya Kijinga Na Wanaume.
Yawezekana Kabla Ya Kuchumbiwa Marafiki Zako Wakubwa Walikuwa Wanaume
(Wapo Wanawake Wa Aina Hiyo). Unachotakiwa Kufahamu Ni Kwamba Hakuna
Mwanaume Anayefurahia Ukaribu Wa Mchumba Wake Kwa Wanaume Wengine.
Hata Kama Hakuna Uhusiano Wa Kimapenzi Lakini Epuka Sana Kujichekelesha
Kwao, Kuongozana Nao, Kukaa Nao Au Hata Kuwasiliana Nao. Ukifanya Hivyo
Utakuwa Unamkwaza Mchumba Wako Na Inaweza Kuwa Moja Ya Sababu Za
Kukuchenga.
2. Marafiki Micharuko
Ukishachumbiwa, Kuna
Marafiki Zako Ambao ‘Automatikale’ Unatakiwa Kuachana Nao. Nazungumzia
Wale Micharuko Ambao Hawawezi Kukushauri Vizuri Juu Ya Maisha Yako.
Hata Wale Ambao Wamekuwa Wakikushawishi Kila Wikiendi Muende Mkajirushe,
Baada Ya Kuchumbiwa Unatakiwa Kujiweka Mbali Nao Ili Kumpa Amani
Mchumba Wako.
3. Tabia Za Kisichana
Ukishachumbiwa
Wewe Si Msichana Tena, Utakuwa Ni Mama Mtarajiwa Wa Familia Yako. Tabia
Za Kisichana Kama Vile Kuvaa Mavazi Yasiyo Ya Heshima, Kukaa Vijiweni
Kuongea Mambo Ya Umbeya Na Nyinginezo Kama Hizo Hutakiwi Kuendelea Kuwa
Nazo.
4. Kujifanyisha
Alichokupendea Huyo Mchumba Wako
Anakijua Mwenyewe, Kwa Maana Hiyo Unatakiwa Kuendelea Kubaki Wewe Kama
Wewe. Usijifanyishe Kwa Namna Yoyote Kama Ambavyo Baadhi Ya Wasichana
Wamekuwa Wakifanya.
5. Eti Umeshaolewa
Kuolewa Ni
Mpaka Pale Mtakapoingia Kanisani, Msikitini Nk Na Kufungishwa Ndoa. Kama
Bado Hamjafika Huko, Wewe Bado Ni Mchumba Tu Na Hata Kwenye Ndoa
Unaweza Usifike.
Kwa Maana Hiyo Hutakiwi Kuhamia Kwa Mwanaume Kama
Ambavyo Baadhi Wamekuwa Wakifanya. Unachotakiwa Kufahamu Ni Kwamba
Kitendo Cha Wewe Kuchumbiwa Kisha Kuamua Kubeba Virago Vyako Na Kwenda
Kuishi Na Mwanaume Ni Kuwakosea Wazazi.
Msomaji Wangu, Yapo
Mengi Ya Kuepuka Mara Tu Unapochumbiwa Lakini Haya Machache Yanatosha
Kwa Leo. Jiangalie Tabia Zako, Zile Ambazo Unajua Wanaume Wengi
Haziwafurahishi, Jiepushe Nazo Ili Kumjengea Mchumba Wako Mazingira Ya
Kukamilisha Taratibu Za Ndoa Yenu.... Nyt! Nyt!
0 comments:
Post a Comment